MwanzoUSD / JPY • Sarafu
add
USD / JPY
Bei iliyotangulia
155.75
Habari kuhusu Dola ya Marekani
Kulingana na takwimu
Kuhusu Dola ya Marekani
Dolar ya Marekani ni pesa halali ya Marekani. Alama yake ni $.
Dolar ya Marekani inapatikana kwa noti za dola 1, 2, 5, 10, 20, 50 na 100. Kuna pia sarafu ya dola 1.
Dolar moja ina senti 100. Senti huitwa pia "penny" nchini Marekani. Kuna sarafu za nusu dolar, robo dolar na sarafu za senti 10, 5 na 1.
Hadi mwaka 1969 noti ya dolar ya Marekani ilikuwa na ahadi ya kwamba serikali ya Marekani itampatia kila mtu dhahabu kulingana na thamani ya dola hizi akipenda kuzibadilisha.
Usawa huu na thamani ya dhahabu ulifutwa. Leo hii dolar ya Marekani ni pesa ya kuiamini serikali kama pesa zote. Maana yake watumiaji husadiki ya kwamba serikali haitachapisha dola kushinda uwezo wa uchumi na thamani ya bidhaa zilizopo nchini Tanzania.
Tangu mwisho wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia dolar ya Marekani imekuwa pesa kuu duniani na sehemu kubwa ya biashara ya kimataifa hukadiriwa kwa dolar hizo. Lakini tangu kupatikana kwa Euro mwaka 1999 umuhimu wa dolar ya Marekani imeanza kupungua polepole. Hata hivyo nchi mbalimbali zimeachana na sarafu zao na kuamua kutumia dolar ya Marekani tu, k.mf. El Salvador. WikipediaKuhusu Yen ya Japani
Yen ni pesa nchini Japani. Alama yake ya kimataifa ni ¥ lakini Japani penyewe huandikwa 円. Yen imekuwa pesa inayotumiwa sana duniani baada ya dolar na euro.
Pesa hii ilianzishwa mwaka 1871 na serikali ya Meiji ikifuata mifano ya pesa za Ulaya. Mwanzoni ililinganishwa na gramu 1.5 za dhahabu.
Thamani ya pesa ilishuka wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia na baada ya vita kiwango chake kwa dollar ya Marekani kiliweka kwa ¥360 kwa US$1. Mwaka 2008 ilikuwa ¥104 kwa US$1.
Tangu kuimarika kwa uchumi wa Japani Yen imekuwa pesa muhimu duniani.
Kuna noti za Yen 1,000, 2,000, 5,000 na 10,000. Wikipedia